Picha za kupigwa kutoka angani kwa kutumia ndege ndogo zisizo na rubani maarufu kama drone zimefichua tofauti kubwa iliyopo baina ya matajiri na maskini ambao ni majirani katika miji mingi duniani.
Mpiga picha Johnny Miller amefichua tofauti kubwa ya makazi na maisha kati ya maskini na mabwanyenye katika miji iliyo Afrika Kusini, Mexico na India.
Picha hizi zingepigwa Dar es Salaam, Mombasa, Nairobi na Mwanza au Dodoma taswira ingekuwa tofauti?
Picha hizo ni sehemu ya mradi wa Bw Miller wa Taswira Zisizo Sawa ambao aliuanzisha Aprili 2016 kuwahamasisha watu kutokubali tena ukosefu wa usawa katika jamii.
Mpiga picha huyo mwenye makao yake Afrika Kusini anasema: "Punde tu unapotua Cape Town, unazingirwa na vibanda na makazi duni.
"Vyumba vya maskini huuzingira uwanja wa ndege, ambavyo inakulazimu kupitia katikati ya vyumba hivyo kwa dakika kumi hivi ukitumia gari kabla ya kufika maeneo wanamoishi watu matajiri na watu wengine wenye mapato ya wastani, maeneo wanamoishi watu waliobahatika (mimi nikiwemo)."
Bw Miller anaendelea: "Hii ndiyo hali halisi ya mambo yalivyo Cape Town, Afrika Kusini, na katika maeneo mengi duniani, lakini ni hali ambayo hainipendezi kamwe.
"Kwa kumnukuu Barack Obama, ninaamini kwamba ukosefu wa usawa na changamoto ambayo kizazi za sasa kinafaa kukabiliana nayo."
Picha za kupigwa kutoka juu angani, zinaonesha vitu vinavyowatenganisha maskini na matajiri.
Wakati mwingine ni barabara, kwingine ukuta au uzio na kwingine ni chemchemi au mto au bahari. Upande mmoja kuna majengo duni na upande ule mwingine majengo ya kifahari.
Ili kupata maeneo mazuri ya kupigia picha zake, Bw Miller hufanya utafiti sana.
Hutumia picha za awali, takwimu kutoka kwa sensa, taarifa katika vyombo vya habari na pia kuzungumza na watu.
"Ninapotambua maeneo ninayotaka kupiga picha zangu, huwa naangalia muonekano wake utakuwaje kwa kutumia huduma ya ramani ya Google Earth, na kujaribu kuandaa njia ambayo droni yangu itapitia. Hii ni pamoja na kuzingatia msukumo wa hewa angani, sheria, usalama, muda ambao betri inaweza kudumu ikiwa na chaji, hali ya hewa, ni wakati gani ufaao, na mambo mengine mengi."
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg