YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 5 March 2013

TIZAMA LIVE MDAHALO WA WAGOMBEA URAISI WA KENYA PIA NA UJUMBE WA OBAMA KWA WAKENYA


MDAHALO WA URAIS KENYA

UJUMBE WA OBAMA KWA WAKENYA

KILICHOFANYA UHURU KENYATA AONGOZE KWA KURA MPAKA SASA HIKI HAPA.

Ongeza kichwa


BREAKING NEWS!!!!! HUGO CHAVEZ AFARIKI


Rais wa Venezuela Hugo Chavez afariki

 5 Machi, 2013 - Saa 23:07 GMT
Wafuasi wa Hugo Chavez wamekuwa wakimuombea aweze kuugua pole
Katika taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo Chavez, 58, kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Alirejea , mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea kupokea matibau. Hata hivyo maelezo zaidi hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.
Bwana Chavez amekua uongozini nchini Venezuela kwa miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa yaliyolenga zaidi kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini.

Ujumbe wa Jeshi

Taarifa kutoka kwa jeshi imesema kuwa wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha usalama. Pia jeshi limeahidi kuendelea kuwa waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas Marduro na wakatoa wito kwa raia kuwa watulivu.

Chavez - wasifu


Hugo Chavez alijitosa katika siasa za Venezuela mnamo Februari 1992 akiwa luteni katika jeshi. Aliongoza mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo Carlos Andres Perez.
Lakini kutokana na kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo wenzake walishindwa kunyakua madaraka hayo. Alikiri kushindwa na aliwekwa korokoroni.
Aliingia uongozini baada ya ushindi mkubwa ulioviondosha vyama vya kisiasa wakati huo. Katika kuapishwa kwake mnamo February 1999, Hugo Chavez alitangaza wazi kwamba mipango yake ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi sio kampeni tu. Alitimiza ahadi yake na kuiongoza nchi hiyo katika mabadiliko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika muda wa miongo kadhaa. Alibadili muundo wa bunge na kulifanya kuwa la kikatiba, ambalo liliiunda katiba mpya baada ya kura ya maoni iliyoidhinishwa na 88% ya wapiga kura.
Rais Chavez alitaifisha rasilmali ukiwemo utajiri wake mkubwa wa mafuta. Sera kama hizi zilimfanya azozane na kampuni za kimataifa za mafuta, lakini alipata uungwaji mkono mkubwa wa watu maskini.

uhuru kenyata bado anaongozza kwa matokeo ya awali

MTANDAO WA GOOGLE ULIMUENZI MIRIAM MAKEBA KWA KUFANYA HIVI.


2
.
.
Kwa kumuenzi staa wa muziki kutoka Afrika Kusini ambae ni mshindi wa tuzo ya Grammy, Marehemu Miriam Makeba.. Mtandao wa Google uliamua kumuenzi kwenye siku yake ya kuzaliwa ambayo ni March 4 2013 ambapo kama angekua hai angekua amefikisha miaka 81.
Google waliamua kuweka mchoro kumuenzi staa huyu kwenye search engine na kuziba herufi g kwa mchoro wa Miriam Makeba ambae alifariki kutokana na mshtuko wa moyo mwaka 2008 akiwa kwenye tour Italia.

MTANDAO WA GOOGLE ULIMUENZI MIRIAM MAKEBA KWA KUFANYA HIVI.


2
.
.
Kwa kumuenzi staa wa muziki kutoka Afrika Kusini ambae ni mshindi wa tuzo ya Grammy, Marehemu Miriam Makeba.. Mtandao wa Google uliamua kumuenzi kwenye siku yake ya kuzaliwa ambayo ni March 4 2013 ambapo kama angekua hai angekua amefikisha miaka 81.
Google waliamua kuweka mchoro kumuenzi staa huyu kwenye search engine na kuziba herufi g kwa mchoro wa Miriam Makeba ambae alifariki kutokana na mshtuko wa moyo mwaka 2008 akiwa kwenye tour Italia.

Sunday, 3 March 2013

Matukio punde yanapojiri:Uchaguzi Kenya



 4 Machi, 2013 - Saa 05:31 GMT
Wapiga kura tayari kwa foleni katika mtaa wa Kibera
Hii leo wakenya wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria chini ya katiba mpya. Foleni tayari zimeanza kushuhudiwa katika vituo.
Kinyang'anyiro ni kikali kati ya Muungano wa Cord na Jubilee wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.
Kwenye ukurasa huu tutakupasha matukio kila yanapojiri hadi upigaji kura utakapokamilika mwendo wa saa kumi na moja jioni.
Unaweza kututumia maoni yako kuhusu uchaguzi unavyokenda kwenye ukursa awetu wa Bofyafacebook

08:30 @smugera anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12 minutes. #bbcnewsday
08:25 Hassan Majid pia mwandishi wa BBC anasema kuwa polisi wamepata mwili mmoja wa mtu aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa panga katika eneo la Moshomoroni

08:24 Mwandishi wa BBC mjini Mombasa, Karen Allen anasema kuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne ambao wameuawa katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa Mombasa. Hana taarifa zaidi kwa sasa

08:16:Frawaso Kimutai kupitia Bofyafacebook yuko katika kituo cha Menengai mjini Nakuru kura ilianza kupigwa saa moja asubuhi na foleni ni ndefu ingawa inakwenda polepole mwendo wa kobe
08:15: Fatma Sanbur yuko mtaani Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga foleni. Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina na hata baada ya saa moja tangu waanza kupangga foleni saa kumi na moja, shughuli yab upigaji kura ilikuwa haijaanza

07:11 James Mwangi: Kwenye ukurasa wa Facebook wa Bofyabbcswahilianasema yuko kwenye foleni na habanduki
07:14 Hison Nyakundi : Yuko mjini Eldoret kwa Foleni tayari kupiga kuraBofyabbcswahili
07:24 Kips Oscar: Kupitia Facebook yuko katika kaunti ya Marsabit anasema upigaji kura unaendelea bila wasiwasi na kuwa wanatarajia shughuli itakamilika kwa muda bila wasiwasi
Usalama ulidhibitiwa asubuhi na mapema wakati upigaji kura ulipoanza
07:28: Mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta, William Ruro amepiga kura mjini Eldoret

07:32: William Ruto anasema kuwa anajivunia uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa amani licha ya dukuduku la wengi. Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo ya uchaguzi vyovyote matokeo hayo yatakavyokuwa.

07:43 Upiga kura bado haujaanza katika baadhi ya sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika vituo kadhaa tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya kupiga kura zao

07:47 Eco Seyar Papa akiwa mjini Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini Nairobi katika eneo la Dagoreti. Foleni zilianza kupigwa kuanzia saa tisa usiku tangu kuanzishwa kwa demokirasia ncini Kenya watu waeneo hili hawajawai kujitokeza kwa mapenzi kama inavyo onekana.
07:50 Mwandishi wa BBC Ann Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu wakiwa hamasa kupiga kura. Wamepiga foleni tangu saa nane usiku.

Foleni ya watu mjini Mombasa
07:52 Mombasa eneo la Kaloleni mpiga kura mmoja amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani maafisa wa tume ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao

PICHA ZA SEHEMU YA MABADILIKO YA KIWANJA CHA NDEGE MWANZA.

0
.
Huu ni mlango wa kuingilia sehemu ya kusubiria mizigo ya abiria waliokuja na ndege.
.
Sehemu ya kusubiria mizigo, hapa pia ndio watu wanapatumia kutokea na kusubiriwa na waliokuja kuwapokea.
.
.
.
Sehemu ya kusubiria mizigo kwa nje, hapo kwenye baraza ambako kuna watu wengi ndio sehemu ya kutoka abiria ukishachukua mzigo.
.
Ukiwa unakwenda kupanda ndege, hapa ndio unaanzia… zamani ilikua ukiwa unasafiri na anaewasili mnapishana sehemu moja lakini kwa sasa wamepatenganisha, hamuonani kabisa.
.
Sehemu ya kusubiri kwa wanaoondoka, hapa ni kwa nje.

TAARIFA KUHUSU LILE KANISA LA MASHOGA NIGERIA.

0
.
.
Ikiwa ni miezi mitatu tu imepita toka nchi nyingine ambayo ni maarufu Afrika (Kenya) kukumbwa na headlines za kutosha kuhusu raia wake wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kupeana tuzo hadharani na kufanya sherehe, leo tena headlines zimehamia Nigeria.
Ndani ya miaka mitano iliyopita huko Nigeria kulikua na Kanisa ambalo lina waumini wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja tu liitwalo House of Rainbow lakini Kanisa hilo lilipotea baada ya kushambuliwa na wakazi wa Lagos ambao hawapendezwi na ishu za ushoga na usagaji.
Tarehe 3 March 2013 Mtandao maarufu wa Nigeria wa TFJ umeripoti kwamba kanisa hilo limerejea tena kwa kishindo na kuendelea na huduma zake.
Ni kanisa ambalo mwanzilishi wake ni mchungaji Mnigeria ambae ni shoga Rowland Jide Macaulay na imefahamika sasa hivi kwamba kanisa hilo lipo Ghana na Malawi, France, Netherlands, Cote d’Ivoire na Sierra-Leone.

SSTORY KUBWA ZA MAGAZETI YA LEO 4 MARCH 2013


0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

namna ya kuandika wasifu wa kampuni.







  • Jina: Goodlove Herman
    Wadhifa: Mkurugenzi
    Simu: +255712356455
    Tuvuti: jinalako.co.tz
    Anwani ya Posta: SLP 10000, Arusha, Tanzania
    Location: Arusha
    Nchi: Tanzania
    Mkoa: Afrika Mashariki

    weka hapa kama ni kampuni au shirika nk  (kwa sababu ya faragha kupata kibali cha maandishi kutoka kwa wamiliki wa kampuni au unaweza orodhesha kulingana na uzoefu wao, elimu na jinsia nk unaweza baadaye kuwasilisha katika binafsi kwa walengwa orodhesha ya majina)

    weka hapa

    weka jina rasmi la usajili au jina linalotumika hapa

    weka hapa

    weka hapa

    Ardhi
    gari
    ofisi
    mashine
    dhamani za ofisi
    nk

    orodhesha hapa
    Bodi ya wakurugenzi = 7 
    washauri wa kudumu= 3
    maafisa wa kudumu= 4 
    Wafanyakazi wasaidizi = 5 
    washauri shirikishwa= 2 
    washauri wa muda= 1
    wafanyakazi wa muda = 3 
    Kazi Kuu za Kampuni 
    Orodhesha yao hapa

    Orodhesha yao hapa

    Orodhesha yao hapa

    Orodhesha yao hapa

    Orodhesha kazi umefanya mafanikio hapa

    orodhesha ya angalau wateja waliofurahia huduma ya kampuni watatu (3)
    taja marefarii wengine wanaojulikana
    Mfano wa marefarii wazuri ni
    Kutoka katika uanachama wako
    Ushirikiano na taasisi zingine nk