YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 24 August 2014

BOSS AMCHOMA MFANYAKAZI WAKE WA NDANI BAADA YA KUKOJOA KITANDANI PICHA ZA TUKIO ZIKO HAPA.



sad1 300x168 SAD AND GRAPHIC  : JUST LOOK AT WHAT THIS WOMAN DID TO HER HOUSEHELP

Mama mmoja wa kutoka Nigeria amemchoma mfanyakazi wake wa ndani kwa kifaa kiitwacho electric cooker kisa kikiwa ni msichana huyo kukojoa ndani.zingine za alivyo jeruhiwa hizi hapa chini



MWANASOKA MWINGINE AFIA UWANJANI

image

Mwanasoka auawa uwanjani

By Israel Saria on August 24, 2014
Mwanasoka wa Cameroon amefariki dunia baada ya kurushiwa kitu kilichompiga kichwani wakati wa mechi jijini Algiers, Algeria.
Mchezaji huyo wa  JS Kabylie, Albert Ebosse (24) alikuwa mmoja wa walengwa waliotupiwa vitu, ikiwa ni pamoja na mawe kutoka kwa washabiki wao kutokana na kutoridhishwa na walivyocheza dhidi ya  USM Alger waliowafunga nyumbani.
Ilitangazwa kwamba Ebosse alifariki dunia baada ya kuchunguzwa alipofikishwa katika Hospitali ya Tizi Ouzou, mashariki mwa Jiji la Algiers. Mchezaji huyo alifunga bao moja, ambapo timu yake ilipoteza kwa 1-2.
Washabiki walianza kurusha vitu kutoka majukwaani walikokuwa wamekaa wakati wachezaji hao wakienda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mechi. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Algeria imeagiza uchunguzi wa tukio hilo kuanza.
Wakati haijathibitika ni kitu gani hasa kilimgonga mchezaji huyo, madaktari walisema kwamba alipoteza maisha kwa sababu ya jeraha la kichwani. Klabu ya USM Alger imeeleza kusikitishwa na kifo cha mchezaji wa wapinzani wao, ikisema ni kitu cha kushitua na kushangaza.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou ametoa tamko akilaani vurugu hizo, na kutoa pole kwa familia na rafiki wa mchezaji huyo chipukizi aliyekuwa akifurahia kazi yake kwa amani na utulivu kiasi cha kutoka nje ya nchi yake kwa jinsi anavyopenda soka.
Hayatou ameonya kwamba soka ya Afrika haiwezi kuwa mazalia ya vitendo vya kihuni kwa namna yoyote ile, na kwamba wanatarajia hatua kali na za mfano kwa wengine zitachukuliwa dhidi ya wahusika wa fujo hizo.

Manchester United close in on Di Maria

Manchester United close in on Di Maria

FC's Craig Burley analyses where Angel Di Maria will fit in to Manchester United's squad should he sign.

TAZAMA PICHA JINSI MARIO BALOTELI ALIVYOPOKELEWA LIVERPOOL




Mario anakubalika: Balotelli alikutana na mashabiki née ya viwanja vya Melwood baada ya mazungumzo ya uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan
KLABU ya Liverpool imemuahidi maslahi mazuri Mario Balotelli ili kuhakikisha mshambuliaji huyo mtata anapiga mzigo wa uhakika Anfield.
Baada ya Liverpool kukubali kutoa Pauni Milioni 16 za ada ya uhamisho kwa AC Milan kumnunua nyota huyo, ilifanya kikao kizito na Mino Raiola, wakala wa mchezaji huyo, Balotelli alikwenda mjini Manchester jana kufanyiwa vipimo vya afya na baadaye akakutana uso kwa uso na kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers kwa mara ya kwanza. 
Mamia ya mashabiki wa Liverpool yalimlaki wakati anaondoka kwenye viwanja vya mazoezi, Melwood na hakuna shaka atakapata mapokezi mazuri Anfield. 
Mshambuliaji huyo wa Italia atasaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamfanya awe analipwa Pauni zisizopungua 85,000- au 90,000 kwa wiki. Lakini ameahidiwa marupurupu zaidi iwapo atafanya vizuri kazini. 


Balotelli akiondoka Melwood jana baada ya kukamilisha mazungumzo 




Mamia ya mashabiki yalijitokeza kumshangilia Balotelli


Hapa ni wakati Balotelli anawasili Melwood kwa mazungumzo

VILIO NA HUZUNI VYATAWALA WAKATI MIILI YA WATU WALIOKUFA KWENYE NDEGE YA MALAYSIA IKIPOKELEWA!

 
Miili 20 ya wahanga wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Kuala Lumpur
Malaysia iko katika siku ya maombolezi ya kitaifa baada ya kupokea miili 20 ya wahanga wa mkasa wa ndege ya Malaysia MH17 iliyotunguliwa Ukraine mwezi uliopita. Miili ilipokelewa na kupewa heshima za kitaifa.

Majeneza yalikuwa yamefunikwa na bendera za taifa na ilibebwa na wanajeshi kabla ya kusafirishwa kwa magari ya kubeba maiti iliyozipitishwa karibu na mfalme na waziri mkuu kabla ya kukabidhiwa kwa familia husika.
MH17 iliangushwa katika eneo la waasi Mashariki ya Ukraine mwezi uliopita.

Machi mwaka huu ndege nyingine ya Malaysia ilitoweka katika bahari hindi amesema kuwa shirika hilo la ndege linaendelea kutatizwa na matukio hayo mawili.

 
Maombolezi Kuala Lumpur 
Wasafiri wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo ya MH17 walifariki 43 kati yao wakiwa raia wa Malaysia. Ndege iliyobeba miili hiyo ilikuwa imetengwa kwa ajili ya shughuli hiyo kutoka Amsterdam na kutua saa nne saa za huko.Bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kote nchini na dakika moja ya kimya itazingatiwa.

Kikundi kidogo cha wanajeshi wa Malaysia kilienda hadi karibu na ndege hiyo kulinda majeneza hayo yalipokuwa yakitolewa kwa ndege huku magari makubwa meupe ya mazishi yakiwa yamepangwa kuzipokea miili hiyo.
Majeneza yote yamefunikwa kwa bendera ya taifa na miili mitatu ya hiyo 20 imechomwa nchini Uholanzi.

 
Baadhi ya Miili 20 ya wahanga wa ndege ya Malaysia
MH17 imezikwa Kuala Lumpur


New Straits Times ilisema sekta ya uchukuzi ya umma nchini humo ikiwemo ile ya reli ya taifa na reli moja ya Kuala lumpur zitasimamisha shughuli zao kuzingatia dakika mbili za kimya kwa heshima ya wahanga wa mkasa huo.

Vibanda maalum kwenye barabara kuu vitakuwa na ishara za kielektroniki kuwaeleza madereva washuke kutoka kwa magari yao ilikutoa heshima.

Msemaji wa ndege za Malaysia alisema kwamba kampuni hiyo ingepanga kipindi cha maombi ambacho kingefanywa wazi kwa mtu yeyote ili kutoa maombi na heshima zao kwa walioaga.
Akiongeza alisema kwamba kampuni hiyo ya ndege za Malaysia imehuzunishwa sana na tukio hilo la kuogofya .

 Aidha imekuwa muda mrefu wa kungoja kwa familia na marafiki wa wasafiri na wafanyakazi waliokuwa katika ndege MH17.

 
Baadhi ya Miili 20 ya wahanga wa ndege ya Malaysia MH17 imezikwa Kuala Lumpur Hii ni mara ya kwanza Malaysia inaendeleza siku ya maombolezi ya taifa kwa wananchi wa kawaida.Heshima hiyo kitamaduni imekuwa ikipewa familia ya mfalme na wakuu serikalini.

Kufikia sasa waathiriwa 28 wa Malaysia wametambuliwa nchini Uholanzi ambako utafiti wa kimataifa kuhusiana na kuanguka kwa ndege hiyo mashariki mwa Ukraine unaendelezwa.

Zaidi ya majeneza 200 iliyo na mabaki ya waathiriwa kufikia sasa yamepelekwa Uholanzi lakini uchunguzi unazuiliwa na mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali ya Ukraine na waasi yanayoiunga mkono Urusi karibu na eneo ambalo ndege hiyo ilianguka

AJINYONGA MFANYAKAZI WA PERAMIHO HOSPITAL.


Mwili wa Fredrick Mgaya (60) ukiwa unaning’inia katika mti aliojinyongea , Tunaomba radhi kwa picha hii. 
Na Mwandishi wetu Peramiho Songea Mwanaume mmoja Fredrick Mgaya (60), mkazi wa Peramiho, Songea mkoani Ruvuma amejinyonga usiku wa kuamkia leo katika maeneo yaliyo karibu na viwanja vya michezo vya Abasia kijijini Peramiho.Mwanaume huyo aliyekuwa akifanya kazi kitengo cha maabara katika Hospitali ya Peramiho na kustaafu mnamo mwezi aprili mwaka huu amekutwa amejinyonga majira ya asubuhi ya leo.

Marehemu Fredrick Mgaya amekutwa na ujumbe katika mfuko wa shati lake, ulioelezea chanzo kilichopelekea yeye kujitoa uhai. Afande Allen Urio ambaye alikuwa mmoja wa mashuhuda wa kwanza,anasema “ Nilikuwa natoka lindo asubuhi ndipo nikakuta kundi la wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa njiani, nikawauliza kwanini wamesimama badala ya kwenda shule muda ule, ndipo waliponiambia kuna mtu ananing’inia kwenye mti pale.

Nilipofika kwenye mti huu ndipo nilipomkuta mzee wetu Fredrick Mgaya akiwa ameshapoteza maisha.
Ni tukio la kusikitisha sana kwani ni mzee wetu katika jamii ambaye tulikuwa tunaishi naye vizuri. Mbali na migogoro yake na mkewe lakini uamuzi aliouchukuwa unasikitisha na si mzuri kabisa.

Kama mlinda amani katika jamii napenda kuwaasa wananchi wajaribu kutafuta suluhu ya matatizo kwa namna nyingine na sio kwa kujitoa uhai”

Akiongea Hakimu wa mahakama ya mwanzo kijijini Peramiho bi Maria Sambo amesema, ameshaletewa na kusuluhisha migogoro ya ndoa hiyo ya marehemu mara mbili na hadi sasa kuna kesi inayoendelea katika mahakama ya Hakimu mkazi, lakini kwa hali ya kawaida hakudhani kwamba marehemu Fredrick Mgaya angefikia hatua hiyo ya kujitoa uhai.

Nao mashuhuda wa tukio hilo wakiongea kwa masikitiko, wengi wamelaani uamuzi uliofikiwa na mzee Mgaya kwani ni dhahiri alikuwa ni mtu wa watu na pia alikuwa ni tegemeo la familia yake ambayo amewaacha ghafla.

 Uamuzi ambao umesababisha maumivu kwa wanajamii hususan ndugu, jamaa pamoja na marafiki wengi waliokuwa wakimpenda na kushirikiana naye kwa mambo mengi ya kimaisha.

Mwenyekiti wa kijiji cha Peramiho A Bwana Joseph Ngonyani ameonesha masikitiko yake ya dhati kwa kuondokewa na moja ya wazee aliokuwa akiwategemea kwa ushauri katika kijiji chake.
“Tukio hili linagusa sana unajua, kwasababu linahusu mtu wa karibu sana na ambaye tunashinda nae siku zote bila kujua nini kinamsibu na nini anakipanga katika akili yake”.

Ndoa nyingi sana zinasumbuliwa na migogoro ya hapa na pale, hivyo ni vizuri watu wa ustawi wa jamii na asasi zinazohusiana na jamii kujaribu kutoa mafunzo na maelekezo ya jinsi ya kutatua migogoro hiyo ili kuepusha adha kama hii isijitokeze tena ndani ya jamii yetu.
Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo bwana Ignasi Kapinga.

Winfried Thadei Mgaya, mdogo wa marehemu anasema, amepokea tukio hilo kwa mshtuko na kwa majonzi sana. Anapata uchungu sana juu ya msiba wa kaka yake kwani marehemu ameacha watoto wanne ambao bado ni tegemezi pamoja na mjane. Pia amesema mazishi yatafanyika tarehe 7 jumamosi kijijini kwao Madaba, Songea mkoani Ruvuma

MTANGAZAJI MWINGINE TENA AONDOKA RADIO ONE.


DU7C9340
Akiyekuwa mtangazaji wa Redio One katika kipindi cha “Spot Leo” Omary Katanga amefuata nyayo za pacha wake Maulid wa Kitenge aliyejiunga na kituo cha redio (93.7) E FM mapema wiki hii.
 Katanga na Kitenge walikuwa wote Redio One, na wataanza kusikika E FM kesho(Leo) katika kipindi cha michezo cha E Sports, ambacho kitakuwa kikiruka kila siku saa 7:00 – 7:30 usiku.
Watangazaji hao wanajiunga na watangazaji wengine maarufu kama Dennis Ssebo, Dickson Ponnela (Dizzo 1), DJ Majay, na Kanky

VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO 22 AUGUST 2014


 
 
 
 
 
 
 
 
 

HIVI NDIVYO KHALID CHOKORAA ALIVYOKUTWA NA PESA BANDIA


Miongoni mwa waimbaji wa muziki wa bendi ambao miezi michache iliyopita alibadilisha headline mbalimbali baada ya kuingia kwenye ulimwengu wa ngumi za kulipwa kwa Tanzania.


Inasemekana amekamatwa na hizo ambazo ni bandia na baada ya kuhojiwa amekiri kuwa ni yake lakini nae kadai amepewa na mtu asiyemfahamu,kaongea na Soudy Brown.
88.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tabora
Bonyeza play kusikiliza.

MAAJABU YA MWAKA,


Maiti hiyo ikiwa imetolewa nje ya jeneza

Ama kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni....Maiti ya mwanamke iliyozikwa miaka 700 iliyopita yagunduliwa China ikiwa haijaoza. Ipo katika hali nzuri kiasi kwamba bado ina nyusi. Inasemekana alihifadhiwa vizuri na inaonyesha alikuwa ni mtu kutoka katika familia ya ufalme. 
Maiti hiyo iligunduliwa na wafanyakazi wa barabara (wakandarasi) huko China mashariki walipopewa kaziya kupanua barabara katika mji wa Taizhou, Mkoani wa Jiangsu. Wakandarasi hao walitakiwa kuchimba kwenda chini kiasi cha futi 6 ili kumaliza mwinuko uliokuwa katikati ya bara bara ndipo wakakutana kitu wasichotarajia kukikuta.
Walipokuwa wakichimba walikuta kitu kigumu  na baada ya kufanya utafiti wao kidogo ndipo waligundua kuwa kulikuwa kuna kaburi alilozikwa mtu na ndipo wakawaita wataalamu ili kuchunguza zaidi, baada ya hapo wakaamua kuweka wazi juu ya tukio hilo kuwa waligundua kwamba kaburi hilo lilikuwa na umri wa miaka 700. Tazama picha zaidi la sakata hilo hapa chini...
Mkandarasi akijaribu kuvunja zege lililozunguka sanduku lakini kabla hawajajua kuwa kuna maiti
Baada ya kuvunja sanduku hilo la zege
Wakihamaki baada ya kuona kitu ndani ya sanduku
Wakianza kufunua matambara yaliyo ndani ya sanduku yaliyozunguka maiti

YALIYOJIRI FIESTA TANGA, USIKU WA JANA





HUYU NDIE MWANAMKE MWINGINE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI JANA HUKO NJIRO ARUSHA


KUNANI ARUSHA?! Baada ya jana mtoto kuuawa kwa kupigwa risasi huko Arusha. Mwanamke mwingine amepigwa risasi na kuuawa leo hii (Jumamosi) alasiri huko Njiro, Arusha. Taarifa za awali zinaarifu ya kuwa mwanamke huyo alikuwa anashuka kwenye gari yake ghafla wakaja jamaa wa pikipiki wakamshambulia kwa risasi na kukimbia...!
Taarifa zaidi zitawajia kadri tutakavyozipata