Exclusive on millardayo.com tena tunapata nafasi nyingine ya kuyafahamu mambo kadhaa kutoka kwa staa wa muziki aliezaliwa ndani ya ardhi ya Museveni 256 Uganda.
Kama haufahamu ni kwamba Jose Chameleone yuko kwenye top 7 ya wanamuziki wa Afrika Mashariki wenye pesa ndefu pamoja na magari ya kifahari ambapo mpaka sasa anakiri kwamba ana magari yote aliyowahi kuwa na ndoto ya kuyamiliki.
Dr Jose amesema “nina magari ambayo nilikua na ndoto ya kuwa nayo, hiyo Range Rover super charge nimeipenda kwa karibu mwaka mzima na nikawa nakusanya pesa kidogo kidogo mpaka nilipoweza kuinunua hivyo nasubiria mpya yake”
Jose Chamelone ambae utajiri wake unatokana pia na kumiliki nyumba za kupanga na kuuza, mashamba na kuuza simu za mkononi zenye jina lake, amesema magari yake yote ameyaandika jina lake huku nikimkariri akisema “nikiwa mdogo sikupata magari ya kuchezea ambayo huwa wanapewa watoto ndio maana nafanya hivi sasa hivi”
Kwenye line nyingine Mayanja anasisitiza kwamba kwa mwaka analipa kama milioni 5 za kitanzania kwa kwa ajili ya kuandika jina lake kwenye gari badala ya namba na ni kitu ambacho anakifurahia, ni sahihi kwake kutokana na ustaa wake, namba kama hizi unaweza kuziweka pia ukiwa Tanzania na utalipia milioni 5 kwa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg